Chini ya Rais Samia Tanzania imenunua ndege mpya aina ya Boeing 787- 8 Dreamliner, namba 5H-TCR, kutoka Boeing – Marekani. Ndege hii ina uwezo wa viti 262 (C22 + Y240).
Kwa wastani wa safari 1.2 kwa siku na load factor ya 85%, inakadiriwa kubeba takribani 97,500 abiria kwa mwaka.
Ununuzi huu umeongeza jumla ya ndege kutoka 11 hadi 12. Dreamliner hii inaiwezesha Tanzania kufanya safari za moja kwa moja hadi Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati, jambo linaloongeza utalii na uwekezaji.
5. DHC-8 Q400 (Refurbished) – USD 35m ≈ Tsh 82 Bilioni Chini ya Rais Samia Tanzania imenunua ndege mpya aina ya De Havilland Q400 (Refurbished) kupitia TGFA.
Ndege hii inauwezo wa viti 76. Kwa wastani wa safari 4 kwa siku na load factor ya 72%, inakadiriwa kubeba takribani 79,900 abiria kwa mwaka.
Ununuzi huu umeongeza jumla ya ndege kutoka 12 hadi 13. Ndege hii imeimarisha safari za ndani, kuunganisha mikoa ya pembezoni na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.