TANGAZO

TANGAZO

MJUMBE WA MKUTANO MKUU MKOA WA DAR ES SALAAM JANETH MWAMBIJE ATEMBELEA WADAU



Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Ilala, Ndg. Janeth Thomson Mwambije, ametembelea ofisi za wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Kivule,  Douglas Didas Masaburi, na diwani wa kata ya Kivule,Rajabu Manyinya, akiwa kama mdau wa Elimu kwenye kata ya Kivule.

Lengo la matembezi hayo ni kuomba msaada wa upatikanaji wa kompyuta pamoja na mashine ya fotokopi kwa shule za sekondari, za Kerezange, Misitu, Kivule na Abuuy Jumaa, zilizopo kata ya Kivule, Ili kuwa chachu ya ufanyaji wa mitihani ya mara kwa mara kwa wanafunzi, na kuwapa uzoefu wa kujua namna ya kukabiliana na maswali na namna nzuri ya kujibu maswali, ili kuongeza ufaulu zaidi kwenye shule hizo.

Aidha Mwambije amesema anaona matumaini ya upatikanaji wa vifaa hivyo, kwani wadau hao aliowatembelea wanaunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha ufaulu wa wanafunzi shuleni.

Hata hivyo, alifanikiwa kutuma  barua pepe kwenye baadhi ya makampuni ya utengenezaji wa taulo za kike, ili kupendekeza ombi la uwezekano wa uandaaji na upatikanaji wa taulo za kike kwa bei nafuu zaidi, ili kufanikisha wanafunzi wa kike wanaoshindwa kumudu gharama za sasa za taulo za kike, kuweza kupata taulo hizo kwa bei nafuu zaidi ili nao waweze kumudu gharama za taulo za kike na waweze kwenda masomoni wakiwa kwenye siku zao.

Mwambije amekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia maendeleo maeneo mbalimbali nchini akiwa na lengo la kuwa muumini wa Maendeleo kama ilivyo kwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com