TANGAZO

TANGAZO

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo Februari 19, 2026 akiwa na Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wamemtembelea  ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Omari Makame. 

Viongozi hao wa Tume wapo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambapo wametembelea na kukagua maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe unaotarajiwa kufanyika Februari 26, 2026.




Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com