TANGAZO

TANGAZO

SIKU YA MALKIA WA HABARI YAFANA, WAZIRI KAIRUKI ATOBOA SIRI YA KUFANIKIWA



Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki amesema mchango wa wanahabari wanawake ni mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ikiwemo za kimahitaji kwa wanawake.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Kongamano la Malkia wa habari lililoandaliwa na waandishi wa habari wanawake, amesema waandishi wa habari wanawake wanapaswa kutumia vyema kalamu zao kama daraja la changamoto za wananchi na serikali.

Katika upande mwingine Waziri Kairuki amewataka waandishi hao kusimamia kikamilifu vikundi na vyama wanavyoanzisha sambamba na kuleta matokeo chanya.

Aidha Waziri ameongeza kuwa zipo fursa nyingi zilizopo katika tasnia ya habari pamoja na mawasiliano hivyo wanawake wanapaswa kuzichangamkia akisema kuwa serikali ipo tayari kutoa ushirikiano.

Ameongeza kuwa ni vyema kuwa na umoja kwa waandishi wanawake wote waliopata ithibati ili serikali iweze kuwatambua kwa urais. 

Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano hilo, Penina Malundo amesema lengo la kongamano hilo ni kujadili chagamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari wanawake kushirikiana katika shughuli za kijamii na kusaidia kuinua sauti ya wanawake katika vyombo vya habari.

Naye Mhariri wa habari za Siasa kutoka katika gazeti la Mwananchi Lilian Timbuka  amewataka waandishi wanawake kujitokeza kutafuta maarifa katika akili unde badala ya kusubiri mafunzo.

Huku Mhariri Mkuu wa Clouds Media Joyce Shebe akiwaasa wanawake kutafuta mbinu mbalimbali za kupambana na taarifa hasi za mitandaoni.

Aidha Mhariri wa habari wa Gazeti la Tanznia Leo, Marry Geofrey amesema kwa kupitia kongamano hilo wamepata fursa nyingi iliwemo kujisemea changamoto zao zinazowakabili.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com