Hali ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam ni shwari na Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam inaendelea kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu
kupitia taarifa zinazotolewa na wananchi na wadau wengine wa usalama.
Jeshi la Polisi tarehe 20/04/2026 eneo la Ubungo Dar res Salaam
limewakamata watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao ikiwemo kutoa
vitisho na lugha za matusi mazito kwa watu mbalimbali.
Kundi hilo baadhi yao wamebainika ni wafanyakazi wa kampuni ya INNOVIX CALL CO LTD na OTAIGO FINANCIAL SERVICES COMPANY LIMITED inayojishughulisha na ukopeshaji wa pesa kwa njia ya mtandao. Watuhumiwa hao ni pamoja na 1. Renatus Mujwahuzi @migeyo Mkazi wa Mbezi Beach, 2. Odilia Oswin
@ngunga Mkazi wa Goba njia nne, 3. Theresia Brastius @kanu Mkali wa
Mtoni Kijichi na wenzao 34.
Hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria.
Katika kutekeleza na kusimamia mifumo ya haki jinai Polisi Dar es Salaam
kwa mara nyingine inawashukuru wananchi na wadau wengine wa usalama
kwa kuendelea kuwashughulikia watuhumiwa wa vitendo vya kijinai kwa
kutumia mifumo ya kisheria.
Polisi Dar es Salaam ina baadhi ya takwimu za Kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili 2026 ambazo baadhi ya watuhumiwa
waliokamatwa na kufukishwa kwenye mifumo mingine ya kisheria
1walipatikana na hatia.
Watuhumiwa waliopatikana na hatia ni pamoja 1.
Hashimu Kasimu @duma mkazi wa Kimara alihukumiwa na Mahakama ya
Wilaya ya Ubungo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti 2.
Vicent Laurent @ndimbo mkazi wa Urafiki Kinondoni alihukumiwa na Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka 3.
Habibu Nassoro mkazi Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti 4. Ismail Ally @muro Mkazi wa
Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha
miaka 30 jela kwa kosa la kubaka 5.
Nelson Julius mkazi wa Mavurunza
Kimara alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kifungo cha miaka
30 jela kwa kosa la unyang ‘anyi wa kutumia silaha 6. Fadhili Issa mkazi wa
Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha
miaka 30 jela kwa kosa la kubaka 7.
Peniel Jonathan @mtakibaleza mkazi
wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Temeke kifungo cha miaka 30
jela kwa kosa la kubaka 8. Yusuph Iddi mkazi wa Mbagala alihukumiwa na
Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la
kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali
zenye viashiria vya kihalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kwenda
mahakamani kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka na kuonekana.
Imetolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam.
