TANGAZO

TANGAZO

ALIYEFUNGUA AKAUNTI FACEBOOK KWA JINA NA PICHA YA BRIGEDIA WA JKT, ADAKWA NA JESHI LA POLISI







Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Samweli Maro Mwita, Dereva bodaboda na Mkazi wa Majohe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufungua akaunti kupitia Mtandao wa Facebook kwa kutumia jina na picha ya Brigedia Hassan Mabena na kuweka maneno yanayosema"napenda kuwakumbusha kuwa nafasi zimetangazwa na vigezo kamili vipo fata utaratibu wote nawapenda sana vijana" kwa nia ya kufanya utapeli. 

Chanzo cha kukamatwa ni baada ya wataalam wa Jeshi la Polisi wa kuchunguza uhalifu na wahalifu wa mtandaoni kupewa taarifa na kuanza kufuatilia na hatimaye kufanikiwa kumkamata leo Aprili 18,2026. 

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo kwa baadhi ya watu wanaotumia majina na picha za watu wengine wakiwepo viongozi wa serikali na wafanyabiashara kufungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii kuacha tabia hizo kwani ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria kwani halitasita kuendelea kuwasaka na kuwakamata. 

Aidha, linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa makini na kutokuamini kila kinacho andikwa au kutangazwa kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kuthibitisha ukweli wake kutoka vyanzo sahihi ili kuepuka kutapeliwa au kujiingiza kwenye mgogoro na sheria. 

Uchunguzi unakamilishwa ili Samweli Maro Mwita aweze kuchukuliwa hatua zingine za kisheria. 

Imetolewa na; 

Msemaji wa JeshilaPolisi

Makao Makuu yaPolisi

Dodoma,Tanzania