TANGAZO

TANGAZO

UHURU WA DEMOKRASIA USIWE KICHAKA CHA UCHOCHEZI NA MWANYA NA VURUGU


Uhuru wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa sasa umezua mjadala mzito kuhusu mipaka yake, huku kukiwa na hofu kuwa baadhi ya makundi wanautumia uhuru huo kama mwanya wa kupandikiza mbegu za uchochezi na chuki. 

Katika mahojiano maalum kupitia kipindi cha Hotzone kinachorushwa na moja ya televisheni nchini, Janeth Mwambije ameeleza kuwa Tanzania si nchi ya kidikteta, uhuru uliopo unapaswa kutumika kwa tija na si kuleta madhara hasi kwa taifa.

Imebainika kuwa kuna kutoridhishwa kwa kiwango cha juu na mwelekeo wa baadhi ya vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, ambavyo vimetajwa kutumia majukwaa yao kuchochea hali ya sintofahamu. 

Hoja iliyotolewa katika kipindi hiki inasisitiza kuwa, upinzani unapaswa kukubali nafasi yake katika changamoto zilizopita badala ya kujaribu kulazimisha lawama hizo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku ikielezwa kuwa vitendo vyao ndivyo vimekuwa chanzo cha mivutano mingi inayoshuhudiwa.

Uchambuzi huo umekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa, ukosefu wa udikteta nchini ndio unaowapa watu fursa ya kufanya vurugu, kwani katika mifumo ya kidikteta hakuna anayeweza kuthubutu kufanya hivyo.

 Hata hivyo, imesisitizwa kuwa uhai wa demokrasia haupaswi kupimwa kwa kiasi cha vurugu au uchochezi, bali kwa uwezo wa viongozi kukaa meza moja, kuzungumza kwa hoja, na kufikia mustakabali wa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mjenga huyo huo alisema kuwa uhuru una faida na hasara zake, na pale unapotumika vibaya, matokeo yake huwa ni maumivu kwa jamii nzima. 

Hivyo viongozi wa kisiasa nchini wametakiwa kuacha kutumia demokrasia kama kisingizio cha kuvuruga amani, na badala yake wajikite katika siasa za kistaarabu zinazozingatia ukweli na kuheshimu mamlaka zilizopo kwa maslahi ya Tanzania.