TANGAZO

TANGAZO

WAATHIRIKA WAKUBWA WA UGONJWA WA MOYO NI WANAUME -DKT. KISENGE




Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amesema kuwa barani Afrika Wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuathirika na magonjwa ya moyo kutokana nakuchelewa kwenda hospitali na kutokana Hali ya Maisha uchunguzi unaonyesha hiyo.

Ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma akizungumza na waandishi wa habari kutangaza miradi ya maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/2026.

Dkt. Kisenge alieleza kuwa sababu nyingine ni uvutaji wa sigara na kutofanya mazoezi ya mwili huku waathirika wengi wao ni kwanzia umri wa miaka 45 na kuendelea.

"Kwetu Afrika kundi linaloongoza ni Wanaume kwasababu wanachelewa kwenda hospital ila wanawake wanawahi pia kundi kubwa la wanaovuta sigara ni wanaume kuliko wanawake" amesema Kisenge.

Aidha amesema ukubwa matatizo unazidi kuongezeka kutoka 1400 mpaka 1500 kwa wagonjwa wa siku huku akisema kila mwezi Taasisi hiyo ina samehe Milioni 200 za matibabu.

Pia amewataka wananchi kuwa na Bima za afya ili kuweza kupunguza gharama za matibabu hayo kwani gharama ni kubwa

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com