Tarehe 07 Septemba, 2026 saa 07:40 usiku katika barabara ya Bagamoyo eneo la Bunju Sokoni Kinondoni Dar es Salaam basi lenye namba T 235 EMJ aina ya Yutong mali ya kampuni ya Abood iliyokuwa ikiendeshwa na Christivian Steven Shemuhilu Miaka 38, mkazi wa Kange Tanga likitokea Tegeta kuelekea Bunju kwa safari ya kwenda Mkoani Tanga iligongana na gari namba T 274 ERU aina ya Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Hamad Mohamed Juma @majid miaka 37, Mkazi wa Mtoni Mtongani Dar es salaam.
Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi kuyapita magari mengine "Overtake" bila ya kuchukua tahadhari ya watumiaji wengine wa barabara na kusababisha vifo vya, Hamad Mohamed Juma @majid miaka 37, Mkazi wa Mtoni Mtongani Dar es salaam, Edward Kimanyara, mstaafu, mkazi wa Yombo Dovya Temeke Dar es Salaam, Magdalena Manyenga, miaka 45, mkazi wa Temeke Dar es Salaam na Melina Emmanuel Kayoka miaka 42, mkazi wa Yombo Kisiwani Temeke Dar es Salaam. Mili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni Dar es Salaam.
Dereva wa basi namba T 235 EMJ aina ya Yutong anashikiliwa kwa hatua nyingine za kisheria.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wote wa barabara wakiwemo waendesha vyombo vya moto kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuzuia na kuepusha ajali.
Imetolewa na:-
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi,
Dar es Salaam.
