TANGAZO

TANGAZO

SPIKA ZUNGU ACHAGULIWA KUONGOZA MKUTANO WA IPU UNAOENDELEA ARUSHA


Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani limechagua Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa umoja huo unaoendelea jijini Arusha.



Hoja ya kumchagua Spika Zungu kuwa Rais wa mkutano huo, imetolewa na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingeza (House of Commons) Sir Lindsay Hoyle na kuungwa mkono na nchi za Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu.