TANGAZO

TANGAZO

𝑴𝑨𝑲𝑨𝑴𝑼 𝑾𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺 𝑨𝑻𝑨𝑲𝑨 𝑴𝑨𝑷𝑨𝑻𝑶 𝒀𝑨 𝑵𝑫𝑨𝑵𝑰 𝑲𝑼𝑯𝑨𝑹𝑨𝑲𝑰𝑺𝑯𝑨 𝑼𝑱𝑬𝑵𝒁𝑰 𝑾𝑨 𝑯𝑶𝑺𝑷𝑰𝑻𝑨𝑳𝑰 𝒀𝑨 𝑴𝑩𝑰𝑵𝑮𝑨

 



Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga wenye thamani ya Shilingi bilioni 3.7, ambapo majengo 15 kati ya 29 yamekamilika tangu mradi huo uanze mwaka 2021.





Katika ziara hiyo, ameuagiza uongozi wa Halmashauri kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani, yanayofikia wastani wa Shilingi bilioni 14.7 kwa mwaka, kuharakisha ukamilishaji wa baadhi ya majengo hasa nyumba za wafanyakazi badala ya kutegemea fedha za Serikali Kuu pekee.





Aidha, amepongeza mafanikio katika kuboresha huduma za uzazi na kupunguza vifo vya mama na mtoto vilivyoripotiwa hospitalini hapo kutoka 550 Kabla ya ujenzi wa hospitali hiyo hadi 106 tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma. Akieleza sababu za idadi ya Vifo, Mganga Mkuu katika hospitali hiyo amesema idadi kubwa ya Vifo inatokana na wajawazito kujifungulia nyumbani.


Akifikisha salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wagonjwa, Makamu wa Rais amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za afya ili kulinda maisha ya mama na mtoto.