TANGAZO

TANGAZO

𝐌𝐀𝐊𝐀𝐌𝐔 𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐀𝐆𝐈𝐙𝐀 𝐓𝐀𝐊𝐔𝐊𝐔𝐑𝐔 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐍𝐆𝐔𝐙𝐈 𝐌𝐈𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐂𝐓𝐈𝐂, 𝐌𝐓𝐖𝐀𝐑𝐀, 𝐌𝐊𝐀𝐍𝐃𝐀𝐑𝐀𝐒𝐈 𝐀𝐃𝐀𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐎𝐒𝐀 𝐔𝐖𝐄𝐙𝐎

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza TAKUKURU mkoani Mtwara kuchunguza mchakato wa utoaji wa tenda ya shilingi bilioni 27, namna mkandarasi alivyopatikana na walioidhinisha tenda hiyo, baada ya kutoridhishwa na kasi na kiwango cha utekelezaji wa miradi ya uboreshajiMiundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) Mkoa wa Mtwara, licha ya mkandarasi kulipwa TSh bilioni 4 za awali.

Tenda hiyo inahusisha ujenzi wa soko, barabara yenye urefu wa kilomita mbili, mtaro mkubwa wa maji na eneo la wajasiriamali.

Akijibu maswali ya Makamu wa Rais kuhusu mwenendo wa mradi, mshauri wa mradi kutoka Norplan (T) Ltd JV Typsa amesema tangu mwanzo mkandarasi kampuni ya Serengeti LTD alionyesha kutokuwa na uwezo wa kutekeleza kazi, huku akiwa na vifaa duni.

Mshauri huyo amekiri kuwa baadhi ya kazi hazijaanza kabisa na kwamba kiwango cha kazi zilizofanyika hakiendani na fedha.

Kufuatia hali hiyo, Makamu wa Rais ameagiza ujenzi wa miradi hiyo ukamilike ifikapo Machi Mosi, 2027, bila nyongeza ya muda. Ameelekeza kuwa mkandarasi akishindwa kukamilisha kazi kwa wakati, atozwe fidia ya ucheleweshaji (liquidated damages) na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.