Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) imeibuka mshindi wa tatu katika kipengele cha Mashirika ya Umma yanayotoa huduma na kufanya Biashara (State-Owned Enterprises Semi- Commercial) kwenye tuzo za Kitaifa zinazohusu taarifa za Fedha zilizowasilishwa kwa Bora mwaka 2024/2025 na kutolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Naibu Kamishna wa Uhifadhi Huduma za Shirika Ngorongoro Aidan Makalla amesema NBAA imetoa tuzo hiyo kwa Ngorongoro baada ya kufuata vigezo, miongozo na viwango vya kimataifa katika uwasilishaji wa taarifa za Fedha. Aidha ameongeza kuwa tuzo hiyo pamoja na kuipa heshima Ngorongoro pia imetoa changamoto kwa Mamlaka kuendelea kutoa taarifa za Fedha zenye ubora wa kimataifa kila mwaka.
*Vigezo vinavyozingatiwa katika utoaji wa tuzo hizo* ni uzingatiaji wa viwango vya uhasibu vinavyozingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia taasisi, Ubora wa muonekano, mpangilio, usanifu na usomaji wa taarifa.
Vigezo vingine vilivyozingatiwa ni ukamilifu wa taarifa za fedha zinazotakiwa kwa mujibu wa viwango bora na ukamilifu wa taarifa za ufafanuzi (*Notes to Financial Statements*), usahihi, uwazi na ufafanuzi wa sera na makadirio ya kihasibu, usanifu a ulinganifu wa Takwimu na taarifa katika sehemu mbalimbali za ripoti.
Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo alikuwa *Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nsubil Joshua* alieleza kuwa Kiwango cha uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa taarifa na mifumo ya udhibiti wa ndani zimeiwezesha *Ngorongoro* na taasisi zingine kukwaa tuzo hizo



