- Atoa maagizo kwa wizara kuchukua hatua
- Asisitiza CCM ni kimbilio la wanyonge
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wassira, ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhakikisha ardhi ya vijiji iliyoporwa kinyume cha sheria, inarudishwa kwa wananchi.
Wasira alitoa maagizo hayo Leo Januari 23, 2025 jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanaCCM waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM.
Alisema Sheria ya Ardhi ya Vijiji inazuia ardhi kuwa bidhaa ya kununua na kuuza kwa sababu ukiruhusu hali hiyo, kuna watu watakosa hata sehemu za kulala.
"Wapo watu wajanja, sheria ile inasema ukitaka ardhi ya kijiji zaidi ya ekari 25 lazima wanakijiji wakutane waandike muhtasari waseme tumekubali.
"Lakini hata wakiandika lazima uende halmashauri ya wilaya, kwa Waziri wa Ardhi na faili lifike kwa Rais kisha asaini. Kuna watu wamechukua ardhi huko vijijini na hawana saini ya Rais.

