Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiongozwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Timotheo Mnzava wakiambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana na Naibu wake Mhe. Dunstan Kitandula pia Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Kamishina wa Polisi Benedict Wakulyamba wamekagua ujenzi wa Ofisi mpya za Hifadhi ya Ngorongoro iliyojengwa nje ya Hifadhi.
Utekelezaji wa mradi huo wa gharama ya takribani shilingi bilioni 10. 5 wa Ofisi na miundombinu mbalimbali umefikia asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, 2025.
Kamati ipo katika siku ya pili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya taasisi chini ya Wizara hiyo kwa siku tatu katika Mkoa wa Manyara na Arusha.



