TANGAZO

TANGAZO

ACT WAZALENDO:TUNAWASEMEA WANANCHI NA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO/ WAJIVUNIA KUTIMIZA MIAKA 11


Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo,  Dorothy Semu amesema kuwa Chama hiko kinasherehekea na kujivunia miaka 11 ya Chama hicho ambacho kimeweza kuwasemea Wananchi changamoto zao pamoja na njia za kuzitatua.


Semu ametoa kauli hiyo leo Mei 05,2025 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hakainde Hichilema uliopo kwenye Ofisi za Makao Makuu wakati akizungumza na Wanachama wa Chama hicho baada ya kutimiza miaka 11 tangu kuanzishwa kwake.


"ACT imejenga jukwaa mbadala ambalo ni kimbilio kwa wanasiasa wote ambao wanapenda siasa safi na ambao hawaridhishwi na ukandamizaji wa Demokrasia kwenye vyama vya Siasa", amesema Semu.


Semu amesema kuwa kielekezo Cha mafanikio yao ni kumpokea marehemu Maalim Seif Hamad na Wenzake mwaka 2019kuaminika kwa Chama hiki na jabari la Siasa kwa afrika mashabiki na Duniani kwa ujumla.

"Chama kimetuma salamu kwa vijana kuwa hiki ndio Chama kinachowaamini na tumeendelea kuwapa nafasi vijana kuonyesha Uwezo wao kwenye Uongozi na Mfano mkubwa ni kumchagua katibu Mkuu wa Chama hiki akiwa na miaka 34 hii ni alama ya wazi kwa vijana wote kuwa Chama Cha ACT wazalendo ndio Jukwaa lao", amesema Semu.

Amebainisha kuwa Chama kimejenga jukwaa la wanawake pamoja na kuvunja minyororo ya kukandamizwa kwa demokrasia na kuongoza kwa vitendo kwa kuvunja dhana ya usawa wa jinsia kwa kuhakikisha kuwa Kuna usawa wa kijinsia kwenye vyombo vyote vya maamuzi.

Amesema ni ACT pekee ndio Chama ambacho unaweza kukuta nafasi za kwenye chombo Cha maamuzi Halmashauri kuu,Kamati kuu uchaguzi umefanyika kwa mfumo 50 kwa 50.

Leo Chama cha ACT Wazalendo kimetimiza Miaka 11 tangu kuanzishwa kwake na imejivunia baadhi ya Mafanikio yaliyopatikana kwenye Chama hicho na kwa muda huo.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com