Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea Ubunge katika Jimbo Kikwajuni, Zanzibar kwa mara nyingine.
Mhe. Masauni amechukua na kuirejesha fomu hiyo Juni 30, 2025 kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mjini, Zanzibar Bw. Bilal Hussein Maulid.