TANGAZO

TANGAZO

OKTOBA KURA ZOTE KWA RAIS SAMIA - UMMY MWALIMU

 


Na. Mwandishi Wetu - TANGA

Kazi nzuri na miradi mingi ya Maendeleo iliyotekelezwa katika Jimbo la Tanga Mjini imetengeneza deni kwa wananchi wa Tanga Mjini dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu ambaye pia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2025.


Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM), Ummy Mwalimu, Juni 16, 2025, alipokuwa akitoa hotuba fupi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Tanga. 

Ummy Mwalimu katika Hotuba yake amesema Jimbo la Tanga Mjini limepata miradi mingi na mikubwa ya maendeleo ambayo imetatua kero za wananchi. 

Kwa msingi huo, Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Samia kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu, asiwe na wasiwasi wa kura kwani wananchi wa Tanga Mjini watampa asante yao kwa njia ya kumpigia kura nyingi za kishindo ili aendelee kukaa Ikulu kuwatumikia Watanzania.

"Kwa kazi nzuri zilizofanyika, sisi watu wa Tanga kwakweli hatuna deni na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na Oktoba 2025, watu wa Tanga tutamlipaDk.t. Samia Suluhu Hassan kwa kumrejesha Ikulu," amesema Ummy Mwalimu.

Mwenge wa Uhuru wilayani Tanga umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikijumuisha miradi ya afya, maji, elimu, viwanda na utawala ambapo wananchi wamepongeza miradi hiyo iliyozinduliwa kwani imegusa ustawi na maendeleo yao.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com