Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti,amewaonya wakaziwa wilaya hiyo watakaowaficha Watoto wenye mahitaji maalumwasipate fursa ya elimu na kusema yeyote atakayebainikaatawajibika kulima shamba la hekari tatu, ndani ya wilaya hiyokabla huku taratibu zingine za kisheria zikifuata dhidi yao.
Magoti,alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhi baiskeli ya kitimwendo kwa mtoto Daudi mwenye mahitaji maalum kwa ajiliya kumsaidia kuanza masomo yake ya awali katika wilaya hiyo.
Alisema kuwaficha Watoto wenye ulemavu,kunawanyima fursaza baadae,huku akijitolea mfano kuwa wazazi wake hawakumzuia kupata elimu iliyomfikisha katika nafasi hiyo yaukuu wa wilaya.
Aliongeza kuwa wazazi wote wenye Watoto wenye ulemavuwassiokuwa na uwezo wa kuwapatia kiti mwendo,Watotowao,wanapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya kwaajili ya kusaidiwa waweze kuanza shule Januari 13 mwaka huu.
“Usimfiche mtoto ndani mimi nimesema adhabu ya kwanza ukimficha mtoto mlemavu asiende shule,adhabu ya kwanza nikulima shamba hekatatu hapa kisarawe,mimi sikufichwa nawazazi wangu ndiyo maana leo ninawasaidia wengine”alisemaMagoti.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa shule za msingi naSekondari wasiwazuie wanafunzi kuhudhuria darasani kwasababu ya kukosa sare za shule na badala yakewawapokee,wakati mchakato wa sare ukiendelea.
