TANGAZO

TANGAZO

UHURU NA UMOJA NDIYO NGAO YETU: EVA MDULA AHIMIZA UZALENDO ZAIDI YA ITIKADI ZA VYAMA



Na. Mwandishi wetu

Katika kuelekea kuimarisha misingi ya utaifa, amani, upendo, na umoja vimetajwa kuwa ndivyo vitu pekee vinavyomfanya mwananchi aonekane bora mbele ya jirani yake. 

Akizungumza, Eva Mdula, amebainisha kuwa bila misingi hiyo, uadui unachukua nafasi na kubomoa kile ambacho kimejengwa kwa muda mrefu, huku akisisitiza kuwa amani ndiyo kiunganishi kikuu cha maendeleo ya kijamii.

Kwa mujibu wa Mdula, ngao ya kweli ya Tanzania ni Uhuru na Umoja, mambo ambayo ndiyo yanayowakutanisha Watanzania na kuwafanya waone kuwa wao ni kitu kimoja licha ya tofauti zao. 

Amebainisha kuwa utambulisho wa Mtanzania ni mkubwa kuliko kadi ya kupigia kura, akieleza kuwa taifa ni la watu wote wa itikadi zote, na kuna maelfu ya wananchi wasio na vyama vya siasa lakini wanafurahia maendeleo yanayopatikana nchini kupitia uongozi uliopo.

"Nje ya vyama na mambo mengine, cha kwanza ni kujua kuwa wewe ni mzalendo wa taifa lako la Tanzania. Mshikamano na umoja ndivyo vinavyosaidia taifa letu kusonga mbele na kupendeza zaidi, kwani kinyume na hapo ni uadui ambao hatuuhitaji," alieleza mzalendo huyo. 

Aliongeza kuwa tofauti za kisiasa zisiwe sababu ya kubomoa umoja, kwani kuondoa amani ni kukaribisha machafuko yanayoweza kuathiri makundi ya watu wasio na hatia wakiwemo watoto, na kutoa mwanya kwa maadui wa nje kuingilia utulivu wa nchi.

Mwisho, Mdula ametoa wito kwa Watanzania wote kudumisha uhuru, amani, umoja, na upendo huku wakiweka kando itikadi za vyama kwa maslahi mapana ya nchi. Amesema kuwa vyama pekee siyo Tanzania, bali taifa ni muunganiko wa watu wenye upendo. Alihitimisha kwa kusema kuwa imara ya amani ndiyo urithi mkuu tulioachiwa na waasisi wa taifa letu, na ni wajibu wa kila mmoja kuilinda ngao hiyo kwa wivu mkubwa.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com