TANGAZO

TANGAZO

JOKATE URBAN MWEGELO (JUM) MWANZILISHI WA KIDOTI FOUNDATION AANGAZA JALADA LA UNCUTXTRA TOLEO LA 23 LA UJASIRIAMALI AFRIKA

 


Dar es Salaam, Tanzania Jarida la UncutXtra, chapisho lenye mtazamo wa Afrika nzima linaloangazia mtindo wa maisha, utamaduni na mafanikio ya Waafrika, limemtangaza Jokate Mwegelo kuwa nyota wa jalada la toleo lake la 23, linalobeba dhima ya “Entrepreneurship Edition” Toleo la Ujasiriamali.

Uteuzi wa Jokate kuwa nyota wa jalada unakuja katika toleo linaloadhimisha ujasiriamali, ubunifu, uongozi na ubora wa Waafrika, huku safari yake ikiakisi kwa kiasi kikubwa maudhui na falsafa ya toleo hilo.

Jokate Mwegelo, Mtanzania anayejulikana katika nyanja za ujasiriamali, habari na mawasiliano pamoja na utumishi wa umma, ameendelea kujenga jina lake kupitia kazi na mafanikio yanayomfanya kuwa miongoni mwa wanawake vijana wenye ushawishi kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

ZAIDI YA TAJI

Katika toleo hili, UncutXtra inamwangazia Jokate kupitia makala maalumu yenye kaulimbiu “Beyond the Crown” – Zaidi ya Taji, ikifungua ukurasa mpana wa safari yake na kumtazama zaidi ya historia yake katika ulimwengu wa urembo.

Makala hiyo inaangazia safari yake ya ujasiriamali, uongozi, nidhamu, maono na mchango wake katika jamii, ikieleza namna alivyoweza kujenga nafasi yake katika maeneo mbalimbali na kuwa sauti yenye ushawishi kwa kizazi kipya.

JOKATE KATIKA JALADA LA WAKUU

Jokate sasa anaungana na orodha ya watu mashuhuri waliowahi kuonekana kwenye majalada ya UncutXtra, akiwemo Burna Boy, aliyekuwa nyota wa jalada la toleo la kwanza, pamoja na Ali Nuhu, Jemima Osunde na Uche Montana, aliyekuwa nyota wa jalada la toleo la 22.

Kuwekwa kwake kwenye jalada la toleo hili ni sehemu ya urithi wa UncutXtra wa kuwaangazia watu wanaowakilisha ubora, ushawishi, ubunifu na simulizi halisi za Afrika.

UNCUTXTRA YAFIKA TANZANIA KWA AJILI YA JOKATE

Kwa kuzingatia asili na mazingira halisi ya safari ya Jokate, timu ya uhariri na ubunifu ya UncutXtra ilisafiri hadi Tanzania kwa ajili ya upigaji picha wa jalada pamoja na mahojiano maalumu.

Hatua hiyo imelenga kuhakikisha simulizi ya Jokate inawasilishwa kwa uhalisia, ikitokana na mazingira ambayo yamekuwa sehemu ya safari yake ya maisha, ujasiriamali na uongozi.

Jokate pia amewahi kutambuliwa kupitia majukwaa mbalimbali ya Afrika na kimataifa, ikiwemo kuorodheshwa katika Forbes Africa 30 Under 30 na kutajwa miongoni mwa vijana wenye ushawishi barani Afrika.

TOLEO LINALOIPELEKA SIMULIZI YA TANZANIA DUNIANI

Kupitia jalada hili, Jokate Mwegelo si tu anawakilisha safari yake binafsi, bali pia anaibeba simulizi ya Tanzania na kizazi kipya cha Waafrika wanaojenga, kubuni na kuvuka mipaka.

Kutoka Tanzania hadi kwenye majukwaa ya kimataifa, Jokate anaendelea kuonyesha kwamba hadithi ya mwanamke wa Kiafrika inaweza kuandikwa kwa ujasiri, ubunifu, uongozi na mafanikio.