MKUU wa Wilaya ya Ilala,Mhe Edward Mpogolo, amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuendelea kulinda na kudumisha amani, umoja na mshikamano pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambazo amekuwa akifanya ili kuwaletea maendeleo Wananchi.
Alitoa kauli hiyo Juni 13, 2026 na Mpogolo, alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila, katika Hafla ya Kupokea Ripoti ya Mapendekezo ya Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Alisema chini ya usimamizi wa Rais samia kumefanyika mageuzi mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya sheria, kuanzishwa kwa masoko ya madini na udhibiti wa biashara haramu ya madini, ambayo yameleta tija kubwa kwa wananchi na taifa.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa makusanyo yameongezeka kwa kiwango kikubwa kufikia Sh. Tril1.107 mwaka 204/25 na mpaka kufikia Juni 13 tayari Serikali imekusanya Sh. Tril 1.3. na kusema kwamba hayo ni matunda ya maono ya Rais Samia.
Alisema ili watanzania na wanadar es salaam kuendelea kuvunna fursa zilizopo ni vyema kama wataendelea kudumisha amani na mshikamano ili serikali iweze kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kuweka mazingira safi ya uwekezaji, akisisitiza kuwa hakuna kitakachostawi kama kutakuwa na migongano na vurugu.
Aidha DC Mpogolo alipongeza hatua ya mapendekezo yaliyotolewa na timu ya wataalamu iliyoundwa kuishauri Wizara ya Madini, kuhusu namna ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini kiuchumi.
Pia amesema, utatuzi wa changamoto za mitaji, teknolojia na upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiolojia kwa wachimbaji wadogo wa madini ni hatua muhimu ya kuongeza ajira kwa wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla, kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa Taifa kuelekea Dira 2050.
Alisema kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mitaji na teknolojia, kunafungua fursa za kuongeza uzalishaji ajira na kipato cha Wananchi hususani wakazi wa Dar es Salaam na kuongeza kuwa hiyo ndiyo njia mojawapo ya kupambana na umaskini.
Pia, Mpogolo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleo kuleta fedha nyingi katika hususani Wilaya ya Ilala, akieleza kuwa, fedha hizo zimeendelea kuboresha miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu ya Barabara na kadhalika.
