Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Kamishna wa Polisi Tatu Jumbe amewataka Viongozi wa Zahanati ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia Ukonga Dar es Salaam kuzingatia matumizi sahihi ya jengo la wazazi kwa malengo yaliyokusudiwa.
Wito huo umetolewa Oktoba 15, 2026 wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la wazazi katika zahanati hiyo ambalo limejengwa kwa kutumia mapato ya ndani.
Pia Mrakibu wa Polisi Charles Kabajuguta Mganga Mkuu wa Zahanati ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia Ukonga Dar es Salaam ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, utii na uzalendo kwa kufuata sheria zote zilizowekwa na Wizara ya Afya kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa viwango vya juu ili kuleta matokeo chanya na maendeleo makubwa katika zahanati hiyo.
Kwa upande wake Magreth Sidodo Diwani wa Viti Maalum Kata ya Ukonga amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura kwa kuweza kuwajengea jengo hilo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano pamoja na kulitunza jengo na kulinda vifaa vilivyopo katika hospitali hiyo.
