TANGAZO

TANGAZO

SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI SEKTA YA NISHATI KWA MAKAMPUNI BINAFSI




Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba leo Novemba 3 , 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya FVIS SDN BHD kutoka Malaysia, kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini.


Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Salome amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari kushirikiana na makampuni binafsi kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwekeza na kuendeleza sekta ya nishati.




Amesisitiza kuwa Serikali imefungua milango kwa wawekezaji na ipo tayari kushirikiana na kampuni hiyo katika kuchochea uwekezaji kwenye sekta hiyo. 






Aidha, Serikali itaendelea kuratibu hatua zinazofuata kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA).


Katika hatua nyingine, Mhe. Salome ameeleza kuwa Serikali ina miradi mbalimbali ya kipaumbele katika maeneo ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme ambayo tayari imefanyiwa upembuzi yakinifu (Feasibility Study) pamoja na tathmini ya athari za kimazingira na kijamii (ESIA), hatua inayolenga kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga; Meneja wa TISEZA Kanda ya Kati, Bi. Phina Lyimo, pamoja na maafisa wengine kutoka Wizara ya Nishati.