TANGAZO

TANGAZO

TUZO IMERUDI NYUMBANI, TUPOKEE, TUITUNZE ILETE TUZO NYINGINE - KAMISHNA BADRU





Tuzo ya ubora katika Utalii endelevu na usimamizi wa Uhifadhi iliyotolewa kwa Eneo la hifadhi ya Ngorongoro na Taasisi ya Africa Business Forum and Awards tarehe 17 Oktoba, 2026 imewasili Nchini leo na kupokelewa nyumbani Ngorongoro.





Akiwasili nchini na tuzo hiyo Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa ushindi wa tuzo hiyo kwa Ngorongoro inaashiria mchango chanya wa Ngorongoro na wadau wa Uhifadhi na Utalii ili kuilinda na kuitunza Ngorongoro milele kwani hifadhi hiyo ni fahari ya nchi kama Urithi wa dunia .


“Tuzo hii inatukumbusha *wahifadhi, watalii na wananchi kuwa ni lazima tuwe na uchungu wa kuilinda Ngorongoro katika ramani ya dunia ili iwe na manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo” amesisitiza Kamishna Badru.


Badru ameeleza kuwa

wanyama, malikale, urithi wa utamaduni, misitu, mimea, ndege na mfumo wa ikolojia nzima ni lazima itunzwe kwa Wivu mkubwa ili kuvutia wageni na kuongeza mapato ya nchi.


Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imepata tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa wa kuweza kusimamia uhifadhi na utalii endelevu licha ya kusimamia hifadhi yenye matumizi mseto.