Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amekabidhiwa rasmi tuzo ya kimataifa ya Uhifadhi na Utalii endelevu ambayo eneo la hifadhi ya Ngorongoro limepokea hivi karibuni nchini Ghana.
Akikabidhi tuzo hiyo mbele ya wakurugenzi wa bodi Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amesema tuzo hiyo imetolewa na Africa Business Forum and Awards kutokana na utafiti uliofanyika na kubaini kuwa Hifadhi ya Ngorongoro inafanya vizuri katika shughuli za uhifadhi na utalii endelevu kwenye eneo lake.
Katika salaam zake Jenerali Mabeyo ameipongeza menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo ambayo ni matokeo chanya ya usimamizi wa Uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limekuwa kivutio kikubwa katika uhifadhi na utalii wa wanyamapori , malikale na urthi wa utamadunu na kuwa kimbilio la watalii kutoka kila pembe ya Dunia.

