TANGAZO

TANGAZO

BALOZI LUVANDA AITAKA NCMC KUYAFIKIA MASOKO YA KIMATAIFA




Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amekitaka Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC) kuimarisha na kupanua wigo wa ushiriki wa Tanzania katika masoko ya kimataifa ya kaboni.




Amesema ushiriki huo upewe msukumo kupitia uhifadhi ya mazingira na miradi ya kaboni katika sekta zote za Uchumi wa buluu, misitu, usafirishaji pamoja na nishati mbadala.





Mhe. Balozi Luvanda ameyasema hayo leo Jumatano Machi 04, 2026 wakati wa ziara yake ya kwanza kikazi katika kituo hicho tangu kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo. 

Mhe. Luvanda amesema amefafanua kuwa kituo hicho kina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa kupitia kaboni hivyo ni vyema kuhakikisha inaimarisha na  kujenga uwezo wa Tanzania kunufaika na masoko ya biashara hiyo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni, Bi. Kathryn Kigaraba amesema kituo hicho kitaendelea na usimamizi wa gesi joto na biashara ya kaboni ili kuwa taaasisi muhimu katika mfumo wa kitaifa wa mabadiliko ya tabianchi na masoko ya kaboni. 

Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni kimeanzishwa Kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 ikiwa ni taasisi ya kimkakati ya kitaifa yenye jukumu la kuratibu shughuli zinazohusiana na na biashara ya kaboni. 

Biashara ya Kaboni ni mfumo wa kiuchumi unaoruhusu uuzaji na ununuzi wa Viwango vya Kaboni ambapo lengo lake ni kupunguza gesijoto angani.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com