TANGAZO

TANGAZO

OMR YATWAA USHINDI NAFASI YA TATU KARATA WANAWAKE






Ofisi ya Makamu wa Rais imebuka mshindi wa nafasi ya tatu kupitia mchezo wa karata upande wa wanawake katika Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi, 2026 yanayoendelea Mkoani Njombe.



Mchezaji aliyepeleka shangwe na vijifo kwa Ofisi ya Makamu ni Shinuna Mohamed ambaye alimfunga Annastazia Majenga kutoka Chuo cha Maendeleo ya Mipango Vijijini (IRDP) magoli 2-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika Uwanja wa CCM Sabasaba Mjini hapa.


Akizungumzia ushindi huo baada ya kutangazwa matokeo hayo Aprili 25, 2026, Shinuna ameishukuru menejimenti ya Ofisi hiyo kwa kuthamini michezo na kusema ushindi huo ni wa watumishi wote. 


Amesema ushindi huo ni historia kwake kwani ni mara yake ya kwanza kushiriki michezo mashindano makubwa ya mchezo wa karata kwani ilihitaji kutumia mbinu za ziada kuweza kuwafunga wapinzani wake.


“Timu zote zimejiandaa vyema na mashindano haya, nilitumia uzoefu wangu kwa kusoma mbinu za wapinzani wangu na kuweza kuwafunga...Najivunia mafanikio haya, naahidi kuweka bidii zaidi ili mashindano yajayo nishike nafasi za juu” amesema Shinuna.


Aidha Shinuna amesema mchezo wa karata ni mchezo mgumu kama ilivyo kwa mchezo wa soka kwani unahitaji maandalizi ya kutosha ikiwemo kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuweza kupata matokeo mazuri wakati wa mashindano.


Amesema katika mashindano hayo amekutana na wachezaji wenye uzoefu wa kushiriki mashindano makubwa ikiwemo SHIMIWI hata hivyo alitumia vyema uzoefu alionao kuweza kuwashinda na hatimaye kuibuka na ushindi.


Kwa upande Katibu wa Klabu ya Michezo Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Marwa Nyaisawa amesema ushindi huo ni kielelezo cha ari, mshikamano na juhudi zinaoendelea kuoneshwa na wachezaji wa timu hiyo katika mashindano ya Mei Mosi.

“Kama ulivyoshuhudia tumekuwa na mwendelezo mzuri wa timu yetu katika mashindano ya Mei Mosi, 2026 pamoja na kwamba ni mara yetu ya kushiriki.. Hii inadhihirisha dhamira tuliyojiwekea kama Ofisi” amesema Nyaisawa.


Nyaisawa amesema mashindano ya Mei Mosi, 2026 yamewapa uzoefu na ukomavu kikosi cha timu hiyo katika mikakati yake ya kujiandaa kushiriki mashindano ya michezo mbalimbali katika siku za usoni.


Nafasi ya kwanza katika mchezo wa karata kwa upande wa wanawake imekwenda kwa Malkia Nondo kutoka Mahakama na kwanza kwa wanaume ikichukuliwa na Susu Jeremia kutoka Wizara ya Afya.